Alhamisi , 1st Oct , 2020

Mshambuliaji wa Everton Dominic Calvert-Lewin amesema ni ndoto yake kuichezea timu ya taifa ya England baada ya mshambuliaji huyo kufunga Hat-trick yake ya pili msimu huu kwenye mchezo wa Carabao Cup dhidi ya West Ham.

Dominic Calvert-Lewin amefunga mabao 8 msimu huu kwenye michuano yote

Calvert Lewin amefikisha mabao nane kwenye michezo mitano msimu huu kwenye michuano yote baada ya kufunga mabao matatu dhidi ya West Ham kwenye mchezo amabao Everton iliibuka na ushindi wa mabao 4-1.

Ilikuwa ni mara ya pili msimu huu mshambuliaji huyo anafunnga mabao matatu kwenye mchezo mmoja, alifanya hivyo pia kweye mchezo wa ligi kuu dhidi ya West Bromwich Albion mchezo ambao Everton walishinda mabao 5-2.

baada ya kufunga Hat-trick yake ya pili msimu huu Cavert Lewin amesema

‘Nimesema mara nyingi hapo awali kuwa ni ndoto yangu kucheza timu ya taifa ya England lakini siwezi kudhibiti hilo kwa sasa na ndio maana napambana ili kujitengenezea nafasi’ alisema

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ndio anaongoza kwa kufunga mabao mengi kwenye michuano yote msimu huu akiwazidi wachezaji wote wa timu za ligi kuu England akiwa na mabao 8.

Cavert Lewin anamatumaini juu ya kile alichokifanya mpaka sasa kinaweza kumpa nafasi kuwa sehemu ya kikosi cha kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate anaetarajia kutangaza kikosi hii leo kitakachocheza michezo mitata dhidi ya Wales, Ubeligiji na Denmark.

Mabao matatu ya Cavert Lewin na bao la Richarlison yalitosha kuipa Everton ushindi wa mabao 4-1 na kukata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali na bao la kufutia machozi la West Ham lilifungwa na Robert Snodgrass, mchezo huu wa raundi ya nne ya Carabao Cup ulichezwa katika dimba la nyumbani la Everton Goodison Park