Bruno Lage kocha mpya Wolves

Jumatano , 9th Jun , 2021

Klabu ya Wolves imemtangaza kocha wa zamani wa Benifica Bruno Lage kuwa kocha mpya wa klabu hiyo, akichukua nafasi ya kocha Nuno Santos aliyeondoka klabu hapo mwishoni mwa msimu uliopita wa 2020-21.

Bruno Lage

Lage alikuwa hana kazi tangu mwezi Juni baada ya kuachana na klabu ya Benifica, ambayo aliifundisha kuanzia Januari 19, 2018 mpaka Juni 29, 2021 na alikiongoza kikosi hicho kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Ureno msimu wa 2018-19.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 45, anachukua nafasi ya Raia mwenzake wa Ureno Nuno Espirito Santos ambaye anaondoka kwenye kikosi hicho baada ya kukinoa kwa miaka minne (4). Nuno mpaka anaachana na Wolves amekiongoza kikosi hicho kwenye michezo 199 kwenye michuano yote ambapo alikiongoza kikosi hicho kushinda michezo 95, droo michezo 49 na michezo ya kufunga 55.

Msimu uliopita wa 2020-21 The Wonderers walimaliza nafasi ya 13 wakiwa na alama 45.