Jumatatu , 30th Mei , 2022

Boston Celtcs imefuzu kucheza fainali ya Ligi ya mpira wa kikapu nchini marekani NBA baada ya kushinda mchezo wa 7 (game 7) leo alfajiri kwa alama 100 kwa 96 dhidi ya Miami Heat katika mfululizo wa michezo ya Fainali ukanda wa mashariki.

Boston Celtics wamefuzu fainali ya NBA kwa mara ya 22

Celtics wameshinda michezo 4 kwa 3 kwenye mfululizo wa michezo 7 ya fainali waliocheza na wataminyana na Golden state worriors kwenye mchezo wa fainali. Ni kwa mara ya 22 Celtics wanafuzu kucheza fainali ya NBA wao ni mabingwa mara 17 na mara ya mwisho kutwaa ubingwa ilikuwa mwaka 2008.

Katika mchezo huu wachezaji nyota wa Boston Celtics Marcus Smart amefunga alama 24, pasi za kufunga (Assists) 5 na amechukua rebound 9 nae Jayson Tatum amefunga alama 26, pasi za kufunga 6 na rebound 10.