Jumatano , 1st Jan , 2020

Taarifa zilizochapichwa katika ukurasa wa mtandao wa  instagram wa muigizaji Jimmy Mafufu, zinasema wameondokewa na mmoja wa wasanii wa filamu aitwaye Diana Choudry Nsumba  ambaye amefariki dunia Disemba 31, 2019.

Marehemu msanii Diana Choudry Nsunda

Sababu ya kifo chake inaelezwa kuwa alizidiwa ghafla nyumbani kwake na amefariki akiwa njiani wakati anapelekwa hospitali ya Mwananyamala ili kupatiwa matibabu.

Kupitia picha na maandishi aliyoweka Jimmy Mafufu kupitia post yake ya mtandao wa  Instagram inasema kuwa,

"Diana Choudry Nsumba mimi nilikuwa napenda kukuita Yezebeli kutokana na filamu tuliyowahi kuifanya pamoja zaidi ya miaka kumi iliyopita,  nimestuka sana baada ya kupata taarifa za kifo chako, Mungu pekee ndio anajua zaidi jinsi nilivyoumia" ameandika Jimmy Mafufu

"Tasnia ya filamu imepoteza mtu muhimu lakini mimi nimepoteza dada na rafiki yangu wa moyoni ambaye hata tusipoonana mwaka lakini siku tukikutana tulikuwa kama tulikuwa wote jana tu, maombi yangu ulazwe mahali pema peponi uende mahali penye starehe ukapumzike paradiso kwa amani mpendwa Yezebeli" ameongeza

Ratiba za mazishi zinasema mwili utaagwa  na kuzikwa leo January 1, 2020 katika makaburi ya mburahati, jijini Dar Es Salaam.