Jumatatu , 8th Feb , 2016

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Amosi Mwamakula amewataka waandaaji wa mapambano nchini kumtafutia mapambano ya Kimataifa ili kuweza kujijengea uwezo zaidi.

Mamakula amesema, alishaomba mapambano na mabondia wazoefu hapa nchini ambapo pambano la kwanza aliomba na Simon Zabron jijini Tanga pambano lililoandaliwa na Ally Mwanzoa lakini Zabron hakuonekana ulingoni huku akiwa amechukua hela.

Mwamakula amesema, pambano la pili amepangiwa kupambana na Mohamed Matumla pambano la utangulizi katika pambano la Bondia Francis Cheka na Bondia Muingereza Februari 27 mwaka huu lakini Matumla amekataa kupambana naye na amerudisha hela kwa muandaaji.

Mwamakula amesema, hali ya kukataa mapambano ni chanzo cha kushindwa katika mapambano ya kimataifa kwani mapambano na mabondia wazoefu humjenga bondia kwa ajili ya kufanya viuzuri katika mapambano ya kimataifa.