Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura
Kazi mojawapo wanayopaswa kufanya viongozi hao ni pamoja na kutatua changamoto ambazo wameziona katika kipindi cha mzunguko wa kwanza wa Ligi.
Mtendaji Mkuu wa bodi hiyo Boniface Wambura amesema, wamepitia katika changamoto nyingi hususani kwa upande wa ratiba lakini vilabu vimepambana mpaka hatua ya lala salama ya mzunguko wa kwanza ambapo vilabu vinaelekea katika usajili wa dirisha dogo ambalo ni fursa kwa benchi la ufundi kufanya tathimini ya kuimarisha benchi kuelekea katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Wambura amesema, mzunguko wa kwanza utakamilika Novemba 12 ambapo Novemba 15 mpaka Desemba 15 itakuwa ni dirisha dogo la usajili ambapo mabenchi ya ufundi yatarekebisha mapungufu waliyoyaona katika mzunguko wa kwanza ili kuelekea katika hatua ya lala salama ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara.


