Jumatatu , 8th Feb , 2016

Baada ya kuwa na mzozo wa muda mrefu juu ya uchaguzi wa Chama cha Gofu Wanawake TLGU Baraza la Michezo la Taifa BMT limekivunja chama hicho na kukiunganisha na Chama cha Gofu Tanzania (TGU).

Katibu Mkuu wa BMT, Henry Lihaya amesema TLGU imekuwa na changamoto nyingi katika suala zima la uchaguzi hivyo wanafanya mazungumzo kwa ajili ya kuunganisha TLGU kuwa sehemu ya TGU ili kuweka mchezo huo katika nafasi nzuri kitaifa na kimataifa.

Lihaya amesema, wapo wanawake wengi wanaocheza gofu lakini hawajitolei kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi suala linalochangia kushindwa kupata viongozi wapya watakaoweza kuendelea kuongoza chama hicho.

Zoezi la uchaguzi wa TLGU lilitakiwa kufanyika Augost 15 mwaka juzi lakini zoezi hilo likawa likiahirishwa kutokana na viongozi kushindwa kujitokeza kwa ajili ya kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hicho.