Nusu ya mataifa ya Afrika hayaungi mkono mgombea wa Sheikh Salman anayeungwa mkono na shirikisho la kandanda la Afrika CAF kwenye uchaguzi wa shirikisho la soka Barani Africa CAF.
Mwenyekiti wa shirikisho la kandanda nchini Liberia Musa Bility amekuwa kiongozi wa kwanza kupinga jambo hilo wazi wazi na kusema ameshangazwa na marais wa vyama vya kandanda barani Afrika na kumuhakikishia hawatampigia Sheikh Salman.
CAF ilitangaza Ijumaa kuwa inaunga mkono raia huyo wa Bahraini mkono kinyume na matarajio ya wajumbe wengi waliokuwa wameahidi kusimama nyuma ya mgombea wa pekee wa Afrika Tokyo Sexwale kutoka Afrika Kusini.
Mussa Bility ambaye alikuwa ametangaza kuwania urais wa FIFA kabla ya kuondolewa kwa makosa ya kimaadili, amesema atamuunga mkono mwanamfalme Ali kutoka Jordan.
Bara la Afrika linajumla ya wapiga kura 54 katika shirikisho la soka duniani FIFA lenye wajumbe 209.
Hata hivyo CAF haina uwezo wa kupiga kura yenyewe kwa niaba ya wanachama wake kwa hivyo kila mwanachama ana uwezo wa kupiga kura kwa siri.




.jpg?itok=0CrdpE0P)