Darwin Nunez ana umri wa miaka 22
Klabu ya Benfica ya nchini Ureno imeikataa ofa ya kwanza ya Manchester United ya Pauni million 80 walioiwasilisha kama ada ya uhamisho ya mshambuliaji Darwin Nunez.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Ureno inaripotiwa kuwa Benfica wapo tayari kumuuza mshambuliaji huyo raia wa Uruguay mwenye umri wa miaka 22 kwa ada ya Pauni milioni 88.8 ambayo ni zaidi ya 257,185,430,880. kwa pesa za kitanzania.
Kwingineko klaby ya Tottenham Hotspur ya England imejitoa kwenye kinyanganyiro cha kumuwania mshambuliaji Paulo Dybala ambaye atakuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Juventus ya Italia kumalizika mwishoni mwa mwezi Juni.
Spurs walikuwa tayari kumsajili Dybala lakini mahitaji ya mshahara ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye miaka 28 ni makubwa. Dybala anataka mshahara wa pauni laki 280,000 kwa wiki ambayo ni zaidi ya Milioni 813 kwa pesa za kitanzania.
Klabu za Inter Milan ya Italia na Manchester United ya England nazo zinaripotiwa kuwa zimeonyesha nia yakumsajili Dybala.


