Jumatatu , 18th Sep , 2023

Beki wa kati Azan FC , Abdallah Kheri 'Sebo', atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti lake la mguu wa kulia.

Sebo ameumiza gegedu 'cartilage' ya maungio ya goti lake la mguu wa kulia, ambayo imelika na pia ameumiza mifupa midogo midogo kutokana na mlalo wa goti lake la kulia na tege alilokuwa nalo.

Beki huyo kisiki, amefanyiwa upasuaji huo leo Jumatatu asubuhi, kwenye Hospitali ya Vincent Palloti, jijini Cape Town, Afrika Kusini.

Aidha, Sebo alipata majeraha hayo kwenye mchezo wetu uliopita wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons, tulioshinda mabao 3-1, ambapo alilazimika kutolewa wakati wa mapumziko, nafasi yake ikichukuliwa na Nathan Chilambo.

Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankemwa, aliyeambatana na beki huyo, amesema kuwa Sebo atarejea kwenye soka la ushindani baada ya miezi mitatu ya matibabu ya majeraha yake kumalizika.

"Sebo amefanyiwa upasuaji wa kisasa unaoitwa arthroscopic, ambao wametoa mifupa midogo midogo iliyokuwa imevunjika na kupandikiza gegedu nyingine.