Nyota mpya aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo Philippe Coutinho ndiye alifunga bao la kwanza katika ushindi wa mabao 2-0 huku yeye pamoja na Luis Suarez wakiandika historia baada ya Suarez kutoa pasi ya bao la kwanza kwa Coutinho ndani ya Barcelona kitu ambacho alifanya pia wakati Coutinho anatua Liverpool 2013.
Coutinho ambaye amenunuliwa kwa £ 142m takribani shilingi bilioni 392 alikuwa akicheza mechi yake ya tano akiwa na Barcelona. Coutinho aliposajiliwa Liverpool akitokea Inter Milan pia bao lake la kwanza alipewa pasi na Luis Suarez.
Baada ya ushindi huo wa 2-0 ambapo bao la pili lilifungwa na kiungo Ivan Rakitic, Barcelona sasa wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya kombe hilo kwa mara ya tano ambapo katika mara nne walizofika wamefanikiwa kuibuka mabingwa mara tatu.
Mchezo wa fainali utapigwa April 21 ambapo Barcelona watacheza na Sevilla iliyotinga fainali baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Leganes.

