
Cristiano Ronaldo
Mkataba wa Ronaldo ulikuwa umalizike mwaka 2018, lakini kwa makubaliano yaliyofanywa leo ameongeza miaka mitatu zaidi kuanzia mwaka 2018.
Mara baada ya kusaini mkataba huo, Ronaldo amewachana wanaodai kuwa amezeeka, na kubainisha kuwa ana uwezo wa kuendelea kusakata kabumbu kwa kipindi cha miaka 10 ijayo.
"Kitu pekee ninachohitaji zaidi ni kuendelea kufurahia miaka niliyobakiza kama mchezaji, bado nina miaka 10" Amesema Ronaldo.
Kwa tamko hilo, ni wazi kuwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 31, amepanga kuachana na soka akiwa na umri wa miaka 41.
Alipotakiwa kueleza iwapo atamalizia soka lake klabu hapo, Ronaldo amesema kuwa lolote linawezekana na kwamba hakuna aijuaye kesho.
Nyota huyo aliyeifungia Real Madrid mabao 371 tangu ajiunge nayo akitokea Man United mwaka 2009, amesema "Napenda ieleweke kuwa, ninaongeza miaka mingine mitano Real Madrid, lakini huu hautakuwa mkataba wangu wa mwisho kusaini na klabu hii, nimezungumza mara nyingi kuwa timu hii iko ndani ya moyo wangu, naipenda na ningependa nimalizie soka langu hapa"