
Lionel Messi na baba yake
Jorge Messi alipata ajali baada ya kumgonga mwendesha pikipiki, kijana wa miaka 24 pembezoni mwa barabara.
Kijana huyo alikimbizwa hospitali na gari la Jorge Messi limekamatwa na polisi kwaajili ya ukaguzi wa vibali.
Uchunguzi uliofanyika umeonesha kuwa ajali hiyo haikuwa kubwa lakini kijana aliyegongwa alikuwa akijisikia vibaya kiasi cha kukimbizwa hospitali.
Hakuna kati ya Lionel Messi na baba yake aliyezungumzia suala hilo mpaka sasa.