Jumapili , 11th Feb , 2018

Baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la shirikisho nchini msimu uliopita na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi, hatimaye klabu ya Simba leo inarejea rasmi kwenye michuano ya kimataifa kwa kucheza na Gendarmerie Tnale ya Djibouti.

Ni miaka minne sasa imepita tangu Simba SC ishiriki kwa mara ya mwisho kwenye michuano ya kimataifa ambapo leo itashuka kwenye dimba la taifa jijini Dar es salaam kucheza mchezo wa raundi ya kwanza kombe la shirikisho Africa.

Mchezo wa marudiano utachezwa Djibouti kati ya Februari 20 na 21, 2018 wenyewe utachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi na Kamishna wa mchezo atatokea nchini Rwanda.

Simba SC inaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu kwa alama 41 baada ya michezo 17.

Mara ya mwisho Simba SC kushiriki michuano ya Afrika ilikuwa msimu 2012/13 ambapo ilitolewa raundi ya kwanza tu na Recreativo de Libolo ya Angola kwa jumla ya mabao Simba 5-0, ikifungwa 1-0 Februari 17 Dar es Salaam na 4-0 ugenini  Machi 3.