Ijumaa , 9th Jan , 2015

Azam FC na Yanga SC wameaga michuano ya Kombe la Mpinduzi baada ya kufungwa katika hatua ya Robo fainali, mechi zilizochezwa uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Azam ilifungwa na Mtibwa Sugar kwa mikwaju ya Penati 7-6 kufuatia sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90.

Kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohammed Kasarama alicheza Panati mbili za Kipre Herman Tchetche na ya mlinda lango mwenzake Aishi Manula.

Kwa upande wa Azam, waliofunga Penati ni Agrey Morris, Didier Kavumbagu, Erasto Nyoni, Brian Majwega, John Bocco na Serge Wawa.

Yanga wametolewa na JKU kwa bao 1-0 lililofungwa Dakika ya 72 na Mshambuliaji Amour Omar kwa kupiga Shuti kali lililomshinda Mlinda mlango wa Yanga Ally Mustapha Barthez