Jumatano , 5th Aug , 2020

Uongozi wa Klabu ya Azam Fc umethibitisha kupokea barua kutoka kwa Klabu ya Yanga ambayo ilikua ikiulizia uwezekano wa wanajangwani hao kumsajili kiungo Salum Aboubakar Sure Boy.

Kiungo wa Azam Fc Salum Aboubakar (Pichani) aliyekua akiwaniwa na klabu a Yanga.

Akizungumza na Kipindi cha Michezo cha Kipenga kinachoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa East Africa Radio, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Azam Fc, Zacharia Thabit amesema walipokea barua ya maombi ya Yanga, yakihitaji kujua gharama za kumpata nyota huyo lakini wamewajibu kwamba mchezaji hao hauzwi.

Zaka alienda mbali zaidi na kusema kwamba Sure Boy yupo kwenye mipango yao kwa msimu ujao na hata yeye anafuraha ya kuendelea kuichezea Azam hivyo hawaoni sababu ya kuruhusu uhamisho wake.

Wiki nzima iliyopita kulikua na taarifa kwamba Yanga inahitaji saini ya Sure Boy ambaye ni mtoto wa zamani wa Yanga mzee Aboubakar Salum.