Jumapili , 13th Apr , 2014

Klabu ya soka ya Azam imejihakikishia kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara baada ya kuifunga timu ya Mbeya City goli 2-0,katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya

Mshambuliaji wa Azam, John Bocco akijaribu kumtoka beki wa Mbeya City,Yusuph Abdallah

Klabu ya soka ya Azam imejihakikishia kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara baada ya kuifunga timu ya Mbeya City goli 2-0,katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya

Mara baada ya Mchezo huo,Nimezungumza na Msemaji wa klabu hiyo ya Azam,Jafa Idd Maganga amesema lengo lao limetimia kwa kuongesha ushindani wa kutosha kwa kutofungwa katika michezo yao yote katika ligi na kuwa mabingwa wapya wa mara wa ligi kuu ya soka ya Tanazania bara msimu huu.

Nayo Dar es salaam Young Africans maarufu kama yanga iliyokuwa iking'ang'ana kuutetea ubingwa ilioutwaa msimu uliopita, imeifunga timu ya maafande ya JKT Oljoro kwa magoli 2-1,mchezo uliopigwa katika uwanja wa Kaluta Amri Abeid, jijini Arusha

Michezo mingine katika kuhitimisha ligi hiyo ni wauza mitumba wa Ilala timu ya Asanti united wameilambisha mchanga timu ya Simba kwa goli 1-0, mchezo uliopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam,Ruvu Shooting wameifunga Mtibwa Sugar goli 1-0,na katika dimba la mkwakwani jijini Tanga,Mgambo wametoka sare tasa na Kagera Sugar.