Katika taarifa yake, Afisa habari wa Azam FC, Jaffari Maganga amesema, moja kati ya mikakati yao kwa sasa ni kuwa na kikosi bora kitakachokuwa tishio kama ilivyokuwa msimu wa 2013/14.
Maganga amesema, katika kuhakikisha hilo linafanikiwa watasajili wachezaji wenye uwezo kutoka ndani na nje ya nchi kulingana na mahitaji ya benchi lao la ufundi.
Azam FC tayari imeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Kombe la Kagame ambayo yamepangwa kufanyika mwezi ujao jijini Dar es salaam.

