Jumatatu , 30th Nov , 2015

Vinara wa ligi kuu ya Soka Tanzania Bara Azam FC inatarajia kwenda ziarani Tanga mnamo Desemba 2 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Afisa Habari wa Azam FC Jaffer Iddy Maganga amesema, timu hiyo ikiwa huko itakuwa na michezo miwili ya kirafiki ya kujipima nguvu ambapo wataanza Desemba tatu dhidi ya Mgambo na mchezo wa pili watacheza na timu ya African Sport Desemba tano ambapo mechi zote zitachezwa uwanja wa Mkwakwani.

Azam FC itarejea jijini Dar es salaam mnamo Desemba sita huku mchezaji Pascal Wawa akitarajiwa kutua nchini kesho kujiunga na kambi tayari kwa maandalizi ya ligi kuu Tanzania Bara.