Alhamisi , 13th Jul , 2017

Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' wamenyimwa dhamana kwa kesi inayowakabili, wamerudishwa rumande mpaka Julai 20 mwaka huu uchunguzi utakapokamilika.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Victoria Nongwa ambapo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ambayo mawili kati ya hayo ni ya kutakatisha fedha.

Kutokana na kesi yao ya utakatishaji fedha kutokuwa na dhamana watuhumiwa hao wamerudishwa rumande kwa mara nyingine tena mpaka uchunguzi wa kesi yao utakapokamilika na kupandishwa tena Mahakamani Julai 20 mwaka huu.