Jumatano , 11th Mei , 2022

Mshambuliaji wa Barcelona Pierre-Emerick Aubameyang sasa ameungana na Mephis Depay katika wachezaji wenye magoli mengi zaidi msimu huu katika kikosi cha barcelona.

(Pierre-Emerick Aubameyang)

Aubameyang amefikisha magoli 13 kwa ujumla aliyofunga tangu ajiunge na klabu hiyo mwezi january mwaka huu baada ya kufunga magoli mawili katika mchezo wa jana walioshinda magoli 3 kwa 1 dhidi ya Celta Vigo, akiwa sawa na Memphis Depay aliyefunga goli moja katika mchezo huo naye akifikisha magoli 13. Huku Ousumane Dembele akiongoza kwa kutoa pasi za magoli katika la liga msimu huu akifikisha pasi 13 za mwisho za usaidizi wa magaoli.

(Gari la wagonjwa lilipoingia uwanjani kumchukua Ronald Araujo)

Lakini ushindi huo uligubikwa na na huzuni baada ya mlinzi Ronald Araujo kugongana vichwa na Gavi kitendo kilichofanya Ronald Arauajo kushindwa kuendelea na mchezo baada kupoteza fahamu na kutolewa nje ya uwanja na kupelekwa hospitali kwa gari la wagonjwa katika kipindi cha pili.

Gavi na Araujo waligongana vichwa wakigombea mpira wa juu na baada kuanguka chini Araujo alisimama na kutembea hatua chake kisha alianguka tena na muda si mrefu timu za matibabu za vilabu vyote viwili zilikwenda kutoa huduma kwa beki huyo raia wa Uruguay.

Baadaye uongozi wa Barcelona walitoa taarifa kwamba fahamu zilimrudia beki huyo na kuzinduka wakati alipopelekwa hospitalini.