Jumatano , 26th Oct , 2016

Aliyekuwa mchezaji mashuhuri wa timu ya Brazil Carlos Alberto ,ambaye alikuwa nahodha wa kikosi kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 1970 amefariki akiwa na umri wa miaka 72.

Carlos Alberto, Nahodha wa zamani wa Brazil, akiwa amenyanyua kombe la Dunia 1970

 

Alberto, anakumbukwa, kwa kufunga mojawapo ya mabao mazuri zaidi duniani katika historia ya Kombe la Dunia katika mechi ya fainali dhidi ya Italia mwaka 1970, baada ya kuwachenga mabeki na kufunga kwa mkwaju mkali.

Beki huyo wa kulia Carlos Alberto alicheza mechi 53 katika timu ya taifa ya Brazil na kushinda mataji ya nyumbani akiwa na Fluminense na Santos alikocheza jumla ya mechi 400.