Jumanne , 17th Oct , 2023

Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri kinatarajiwa kuwasili Kesho jumatano ya Oktoba 18 ,2023 jijini Dar es Salaam, tayari kwa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya African Football League dhidi ya Simba SC utakaochezwa siku ya ijumaa hii katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam

Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari Meneja habari na mawasiliano Simba SC Ahmedy Ally  amesema hii  ndio michuano yenye  thamani zaidi barani Afrika na hali ya kikosi inaendelea vyema na mazoezi na kila mchezaji yupo na shauku ya kufanya vizuri katika mchezo huo.

"Maandalizi haya  babkubwa yanayofanyika  kwenda uwanjani. Hakuna Mwanasimba anatakiwa kubaki nyumbani, hiyo siku ni kwenda uwanjani. Historia hiyo itabaki kwa vizazi na vizazi."

"Lazima tuambiane ukweli AFL ya safari hii imeshirikisha timu nane bora na Mnyama yupo kati ya timu hizo bora, AFL zijazo zitakusanva kila mtu ambavo haitakuwa na thamani sawa na hi ya kwanza."- amesema. Ahmed Ally.