Ijumaa , 1st Feb , 2019

Wapinzani wa Simba katika mchezo wa tatu wa kundi D, timu ya Al Ahly ya Misri inatajwa na vyanzo mbalimbali vya rekodi za soka duniani kama miongoni mwa vilabu vitatu vilivyofanikiwa zaidi duniani.

Al Ahly wakishangilia moja ya mataji yao.

Ahly ambao kwa Afrika ndio klabu yenye mafanikio zaidi, kutokana na kuwa mabingwa wa Historia katika kila taji ambalo linatambulika na shirikisho la soka (CAF).

Al Ahly ambayo ilianzishwa April 24 1907, ndio mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Misri wakiwa wametwaa mataji 40.

Barani Afrika Ahly ni mabingwa wa kihistoria wa CAF Champions League wakiwa wametwaa mara 8. Pia wametwaa mara 4 kombe la washindi barani Afrika 'African Cup Winners' ambayo nayo ni zaidi ya klabu yoyote. Pia wana rekodi ya kushinda mataji mengi zaidi ya CAF Super Cup wakiwa wametwa mara 6.

Moja ya vyanzo vya rekodi za soka duniani, mtandao wa (besoccer) unaitaja Al Ahly kuwa klabu ya pili kwa kuchukua mataji mengi zaidi ya kimataifa ikiwa nayo 24, ikizidiwa na Real Madrid yenye 25 huku Barcelona ikiwa ya tatu na mataji 20.

Mataji ambayo Al Ahly imechukua mpaka sasa.

Ligi kuu 40
FA Cup Egypt 36
Egypt Super Cup 10
CAF Champions Legue 8
African Cup Winners 4
CAF Super Cup 6
Jumla 104.

Msimu uliopita walicheza fainali ya Ligi ya mabingwa na kufungwa 3-1 na Esperance ya Tunisia. Jumamosi ya Februari 2 wnaakipiga na mabingwa wa Tanzania Simba mchezo utakaopigwa kuanzia saa 4:00 usiku.