Jumatano , 3rd Dec , 2014

Nahodha wa Klabu ya Yanga Nadir Cannavaro na Mlinda Mlango wa Klabu ya Azam FC Aishi Manula wameingia katika orodha ya wanamichezo wanaotarajiwa kuwania tuzo za wanamichezo bora zinazotarajiwa kufanyika Desemba 12 jijini
Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo hizo, Rehule Nyaulawa amesema tuzo hizo zitashirikisha michezo mbalimbali nchini ambapo Cannavaro atawania tuzo ya mwanasoka bora nchini huku akipambanishwa na wachezaji Elias Maguli ambaye alikuwa Ruvu Shooting na hivi sasa yupo Klabu ya Simba na Erasto Nyoni wa Azam FC.

Nyaulawa amesema Aishi Manula anawania tuzo ya mwanamichezo chipukizi huku akishindana na Sheridah Boniface anayecheza soka la wanawake na Omari Sulle anayecheza mchezo wa Tenis ambapo tuzo ya heshima itatangazwa siku ya ugawaji wa tuzo hizo.