Jumanne , 28th Feb , 2017

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA Gianni Infantino amesema kuwa Afrika itapewa nafasi 7 katika upanuzi wa timu zitakazoshiriki katika Kombe la Dunia mwaka 2026.

Infantino ambaye yuko nchini Ghana kwa ziara ya siku moja, amesema kuwa shirikisho hilo limeongeza uwekezaji wake Afrika kutoka dola milioni 27 hadi 94 kwa mwaka ili kusaidia kukuza mchezo huo.

kufuatia uamuzi huyo mashabiki wa soka nchini wameelezea furaha zao kusema ahueni hiyo inatokana na kwamba angalau wigo utakuwa umeongezeka na kupunguza ugumu wa kuwania nafasi hizo kwa mataifa yote barani Afrika wanachama wa FIFA kuwania nafasi 5 zilizokuwa hapo awali.

Wengi wa mashabiki hao pamoja na kumpongeza Rais wa FIFA lakini wakapendekeza kuwa kutokana na wingi wa wanachama wa FIFA kutoka bara la Afrika ni vyema kila baada ya msimu wa michuano ya kombe la dunia kuwepo na ongezeko la timu mbili ili baadaye Afrika iwe na wawakilishi wengi kama ilivyo kwa bara la Ulaya na America.

Pia mashabiki hao wamesema hii ni bahati kwa Afrika kupata fursa hiyo kutoka kwa Rais mpya wa FIFA kufanikisha jambo hilo japo bado tunahitaji nafasi zaidi ili kupanua wigo wa uwezekano wa kushindana kuwania nafasi ya kucheza hatua ya juu zaidi ya michuano ambayo mara zote mafanikio makubwa kwa Afrika inakuwa kuishia hatua ya robo fainali.