
Akizungumza jijini Dar es salaam, Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Baraka Kizuguto amesema, African Sports waliibuka washindi wa kwanza katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa kwanza Kundi B ambapo watacheza mchezo huo wa fainali na Bingwa atapewa zawadi ya Kombe na medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.
Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza FDL ilimalizika mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi Kuu kwa kila kundi kutoa timu mbili ambapo Kundi A ni African Sports na Majimaji FC, Kundi B ni timu za Mwadui FC na Toto Africans.
Nazo timu za Green Worriors na Villa Squad zimeteremka Daraja la pili baada ya kushika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza, Villa Squad kutoka Kundi A na Green Warriors Kundi B.