Jumatatu , 23rd Jun , 2014

Kamati ya uchaguzi wa klabu ya soka ya Simba uchaguzi ambao uanataraji kufanyika june 29 mwaka huu hii leo imetangaza majina ya mwisho ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu hiyo

Kamati ya uchaguzi ya klabu ya soka ya Simba.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo Dr. Damas Ndumbaro amesema baada ya kamati ya rufaa ya uchaguzi ya shirikisho la mpira Tanzania (TFF) kupitia rufaa mbalimbali, hivyo anatangaza majina rasmi ya wagombea ambao wamepitishwa kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa Simba Sports Club mwaka huu

Ambapo Ndumbaro amesema nafasi ya urais waliopita ni wagombea 2 huku wagombea wanne wakipita kwa nafasi ya makamu wa rais na katika nafasi ya kamati ya utendaji wanaume waliopitishwa ni wagombea 18 huku kwa upande wa wanawake waliopitishwa ni wagombea watatu

na ifuatayo ndio orodha ya majina hayo ya wagombea ambao hii leo wameanza kampeni rasmi baada ya kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba kutangaza rasmi kuanza kwa mchakato huo :-

A. Nafasi ya Rais

1. Andrew Tupa
2. Evans Aveva

B. Nafasi ya Makamu wa Rais

1. Bundala Kabulwa
2. Geofrey Nyange
3. Jamhuri Kihwelo
4. Swedi Mkwabi

C. Nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji (Wanaume)
1.Said Tulliy
2.Yasini Mwete
3. Ally Suru
4. Rodney Chiduo
5. Said Pamba
6. Ally Chaurembo
7. Abdulhamid Mshangama
8. Chano Almasi
9. Damian Manembe
10. Ibrahim Masoud
11. Kajuna Noor
12. Hamisi Mkoma
13. Alfred Elia
14. Saidi Kubenea
15. Idd Mkamballah
16. Juma Mussa
17. Maulid Abdallah
18. Collin Frisch