
Mchezaji wa Yanga, Juma Abdul.
Juma Abdul amesema hayo zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mchezo wa pili wa makundi wa kombe la Shirikisho ambao Yanga itacheza na Gor Mahia July 18.
“ Kitu kikubwa mi ninachoweza kusema ni kuwatoa wasiwasi mashabiki wetu, Yanga ni timu kubwa kwahyo hata kama imefanya vibaya katika ligi kuu wanaweza kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, kikubwa tuu kwa hivi sasa ni kujipanga kuhakikisha tunafanya maandalizi mazuri tukishirikiana na wachezaji watakaosajiliwa ili tuweze kufanya vizuri katika mashindano ya Shirikisho “, amesema Juma Abdul.
Pia Juma Abdul amezungumzia kiwango cha Gor Mahia akisema kuwa wana kiwango kizuri tangu katika mashindano ya mwaka uliopita ya Spoti Pesa ambayo waliweza kuchukua ubingwa na kucheza na Everton.
Yanga ilijiondoa katika michuano ya Kagame siku chache kabla ya kufunguliwa rasmi wakidai wanahitaji muda zaidi wa kujiandaa vizuri na mchezo huo dhidi ya Gor Mahia lakini Gor Mahia wenyewe wakileta timu yao ambayo nayo haikuwa wachezaji wao tegemeo.
Yanga iko katika kundi D pamoja na Rayon Sports ya Rwanda, USM Alger ya Algeria pamoja na Gor Mahia ya Kenya .