Jumatano , 11th Feb , 2015

Timu ya BDF kutoka nchini Botswana inatarajia kuwasili nchini kesho kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa mzunguko wa kwanza Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga mchezo utakaochezwa Jumamosi ya Februari mwaka huu, uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Yanga watacheza huku wakihitaji ushindi mzuri kwa ajili ya kujiweka katika mazingira mazuri kabla ya mchezo wa marudiano hapo baadaye mjini Gaborone.

Katika michuano hiyo, CAF imeamua timu zijilipie malazi zinapokwenda kwenye mechi za ugenini baada ya kuwepo malalamiko timu ngeni kupatiwa Hoteli duni miaka ya nyuma.

Mechi hiyo itachezeshwa na Thierry Nkurunziza akisaidiwa na Ramadhani Nijimbere namba moja, Herve Kakunze namba mbili huku mezani akiwa Gerge Gatogato wote kutoka nchini Burundi wakati kamisaa atakuwa Joseph Nkole wa Zambia.