Alhamisi , 22nd Feb , 2024

Mara baada ya shirika la anga za juu la Marekani (NASA) kutangaza nafasi kwa watu ambao wangependa kujitolea kuwa sehemu ya utafiti muhimu kwenye sayari ya Mars utafiti utakaodumu kwa muda wa siku 365.

Utafiti uliolenga maandalizi ya mwanadamu kuhamia sayari ya Mars, Taarifa ambayo ina siku tatu tangu itolewe kwa umma, Lakini kubwa na la kushangaza mpaka sasa kwenye Dunia ya watu zaidi ya Bilioni 8, watu zaidi ya milioni 24 wameomba kuwa sehemu ya majaribio haya.

Huku China ikiongoza kwa idadi ya watu wengi zaidi waliomba ambao ni watu zaidi ya Milioni 4 ikifatiwa na nchi ya Marekani ambayo ilipata waombaji zaidi ya Milioni 3.