Vera Sidika azima kelele za ujauzito

Jumatatu , 21st Jun , 2021

Vera Sidika imemlazimu kuthibitisha kama kweli ni mjazito kutokana na madai ya watu wengi kuwa ujauzito wake ni bandia (fake).

Picha ya Vera Sidika

Baada ya taarifa za uvumi kuenea sana mitandaoni, Vera amewafunga midomo watu kwa ku-post picha ikionesha ujauzito wake na kuambatanisha ujumbe unaosomeka “kwa hivyo tumbo langu litaonekana kuwa kubwa katika picha zangu zote kwa miezi kadhaa, itabidi selfies pia zikam through”.

Vera Sidika

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii walikuwa wakimkosoa kwa miaka mingi kwa kutopata ujauzito na hatimaye hilo amelifanikisha na mpenzi wake Brown Mauzo.