Jumanne , 30th Nov , 2021

Kama bado hujapata pesa ya kulia bata Christmas na mwaka mpya basi mkwanja huu hapa, kampuni ya kutengeneza maroboti nchini Urusi imetoa ofa ya Tsh million 459 kwa mtu atakayekubali sura na sauti yake itumike kutengenezea roboti.

Kampuni ya Promobot imetangaza kulipa Tsh million 459 kwa mtu atakaewapa idhini ya kutumia sura yake na sauti itumike milele katika kutengeneza maroboti ambayo yatafanya kazi katika mahoteli, mall, na sehemu nyingine zenye mikusanyiko ya watu.

Vigezo vya mtu wanae muitaji lazima awe na sura ya ukarimu na sauti ya upole bila kuangalia umri na jinsia.