Ufahamu wa wananchi kuhusu kupandikiza mbegu

Alhamisi , 13th Mei , 2021

Kufuatia taarifa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanza kutoa huduma ya kupandikiza mbegu za uzazi kwa wanawake wenye uhitaji, EATV & EA Radio Digital imeingia kitaani kupiga stori na raia juu ya maoni yao kuhusu suala hilo.

Picha ya David Moses kushoto, kulia ni Mama Saida

"Hilo suala linanichanganya, kwanza wanapandikiza kwa wanawake ambao ni wajane, wasio na wanaume au wanawake wa mtaani maana ni jambo gumu na hao watoto watakaopandikizwa watakuwa hawana baba au itakuaje, hii ishu inanishtua baada ya kuisikia" David Moses 

"Mimi sipo tayari kupandikiza mbegu zangu kwenye suala la uzazi kwa sababu nitazaa mtoto ambaye hana baba wala ndugu kwa upande wa baba yake, nimeziopokea taarifa hizi kwa watu kama wenye shida ya uzazi, hili suala likiendelea ndoa zitakuwa hakuna tena, maana nikitaji mtoto nitaenda Hospitali kupandikiza" Mama Saida 

"Nimepokea kwa uzuri na ubaya kwa sababu kumpandikiza mbegu mwanamke mtoto akizaliwa huwezi jua mtoto atafanana na nani, pendekezo langu mimi nimjue atakayenipandikiza hizo mbegu hiyo itanisaidia kumjua baba wa mtoto hata kama hatuna mahusiano yoyote" Dada Sestiria