Alhamisi , 20th Nov , 2025

Kuuza siyo tu kuhusu bidhaa nzuri ni kuhusu kuelewa akili ya mteja. Hapa nimekuletea mbinu 7 za kisaikolojia unazoweza kutumia kuongeza mauzo yako kwa kutumia njia rahisi na za kueleweka.

1.    Upungufu (Scarcity) Kuhamasisha wateja kufanya maamuzi haraka kwa kuonesha bidhaa zimebaki chache au ofa inaisha muda si mrefu. WaTanzania hupenda kutokukosa fursa. "Zimebaki Shati 5 tu na Ofa hii mwisho ni kesho’’

2.    Ushahidi wa Kijamii (Social Proof) Kujenga imani kwa kuonesha idadi kubwa ya Watanzania wenzake wametumia na kuridhika. Watu hufuata wanachofanya wengine."Watu 5,000 wameshaagiza.

3.    Mamlaka (Authority) Kuongeza uaminifu na uzito wa bidhaa yako kwa kutumia ushuhuda au mapendekezo kutoka kwa wataalamu au watu maarufu/wazito kwenye jamii. "Imetumika sana na Gwiji wa Bongo Fleva"

4.    Upendeleo (Reciprocity) Kufanya jambo zuri (kama kutoa ushauri au zawadi ndogo) kwanza, na kumfanya mteja ajisikie kuwajibika kurudisha fadhila kwa kununua kwako. Mwanadamu hupendelea kurudisha fadhila pale anapotendewa jambo zuri. Mfano kutokana na aina ya Ngozi ya mteja unampa ushauri wa mafuta ya kutumia.

5.    Punguzo la Bei (Anchoring) Kuonesha mteja kuwa amepata faida kubwa kwa kuweka bei asilia (ya juu) kwanza, kisha kutoa punguzo kubwa. Hii huongeza thamani ya ofa machoni pa mteja. Mfano "Bei Halisi 100,000, leo 45,000 tu!"

6.    Kuibua Hisia (Emotional Triggering) Kuchochea maamuzi ya ununuzi kwa kutumia hadithi au picha zinazogusa moyo wa mteja (furaha, matumaini, hofu). Mfano "Hii itawafanya watoto wako wafurahie uwepo wako kila wakikuona’’.

7.    Uharaka  (Urgency)Kuweka kikomo cha muda ili kuwafanya wateja kuchukua hatua mara moja kabla ofa haijaisha. Mfano "OFA hii ni kwa wiki hii pekee"