Joseph Mbilinyi na mke wake Happiness Msonga
Mmoja wa watu maarufu na mwanasiasa ambaye ni mbunge wa jimbo la Mikumi Mh.Prof Jay amewapa pongezi kwa kupost picha na video katika mitandao ya kijamii ya Instgram na Twitter ambapo ameandika,
"Muda wa kanisani harusi ya Jongwee, Mbeya stand up , Hongereni sana kaka yangu @jongwe__ na Shemeji yetu Happiness msonga kwa kukamilisha ndoa yenu takatifu leo, Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu Awabariki zaidi na awasiamie kwenye Maisha yenu ya NDOA, AMEN"
Mr II Sugu kabla ya kufunga ndoa na mke wake huyu wa sasa alikuwa na mahusiano mfanyabiashara na muigizaji Faiza Ally na walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike.
Mbunge mwingine ambaye amempongeza Sugu ni Mbunge wa Mtama (CCM), Mh Nape Nnauye.
Hongera sana kaka! Karibu kwenye club! Maisha yako yana historia ya kusimulia/ your life has a story to tell! pic.twitter.com/wtYSTEBf5E
— Nape Moses Nnauye (@Nnauye_Nape) August 31, 2019


