
Rais wa Bongo Fleva, Dullah Planet akikabidhiwa funguo ya gari na Mkuu wa Idara ya Masoko wa East Africa Television Ltd, Roy Mbowe.
Kampeni hiyo ni maalumu kwa ajili ya kuwatambulisha vinara wa East Africa Radio katika nyanja mbalimbali kwa wasikilizaji na wafuatiliaji wetu popote walipo duniani.
Akizindua kampeni hiyo, msimamizi wa mkutano wa leo ambaye ni mtayarishaji wa kipindi cha Planet Bongo, Grayson Gideon amesema kampeni itakuwa na mabalozi wanne wa mwanzo ambaye ni Dullah Planet (Rais wa Bongo Fleva), Maryam Kitosi (Mwanamke Kinara), Samson Charles (Mchambuzi Mkuu Siasa) na Ibra Kasuga (Mtaalamu) katika masuala ya michezo.
Kwa nyakati tofauti tofauti, mabalozi hao wameishukuru East Africa Television L.t.d pamoja na East Africa Radio kwa kuanzisha kampeni hiyo na kuahidi kujitoa kwa moyo wote.
"Tumeona kitu kikubwa ambacho Rais @MagufuliJP amefanya jana na mimi kama Rais wa Bongo Fleva nimefurahishwa sana nampongeza kwa juhudi zake. Kubwa zaidi mimi kama Rais wa Bongo Fleva nilikuwa napenda wasanii kuungana. " - @dullah_planet Rais wa Bongo Fleva.#SimamaNaMimi pic.twitter.com/r3z6dbtLsW
— EastAfricaRadio (@earadiofm) July 13, 2020
"Mimi ni Maryam Kitosi, ninashukuru sana kuwa balozi wa wanawake katika kampeni hii. Nimefanya kazi kubwa za wanawake na nina uzoefu na ninafanya kipindi kwa ajili ya wanawake kinaitwa 'MamaMia' nitatoa mchango wangu wote kwenye hili"- @MaryamKitosi Mwanamke Kinara#SimamaNaMimi pic.twitter.com/q277i9vsJ3
— EastAfricaRadio (@earadiofm) July 13, 2020
"Kubwa hasa naweza kusema nimepokea vitabu vyote vya kimbinu na ufundi na nakwenda kama mtaalamu ili kuhakikisha katika suala la michezo tunakwenda mbele. EA Radio na TV tumebarikiwa utajiri wa vipindi vya michezo ambavyo tutavitumia vyema" - Ibrah Kasuga, Mtaalamu#SimamaNaMimi pic.twitter.com/eZ2QW9dTo6
— EastAfricaRadio (@earadiofm) July 13, 2020
Tazama tukio nzima la uzinduzi wa Simama na Mimi hapa chini.