Jumanne , 2nd Aug , 2022

Kampuni ya SBT inayojihusisha na kuagiza magari kutoka nchini Japan wamechangia taulo za kike pakiti 240 kupitia kampeni ya Namthamini siku ya leo ambazo zitakwenda kuwasaidia wanafunzi 20 shuleni kwa mwaka mzima.

Wafanyakazi wa SBT wakikabidhi taulo za kike katika ofisi za East Africa TV na East Africa Radio.

Afisa Mauzo wa kampuni ya SBT, Imelda Koku anasema wameamua kushiriki katika kampeni ya Namthamini kwa sababu wanaelewa jinsi gani wanafunzi wa kike wanavyokuwa na uhitaji wa taulo za kike wanapokuwa mashuleni.

“Tumeamua kuwa katika nafasi hii ya Namthamini kwa sababu tunaelewa jinsi gani wadogo zetu wa kike wanakuwa na uhitaji wanapokuwa mashuleni”