Jumanne , 30th Aug , 2022

Kampuni ya taulo za kike ya QiPads siku ya leo imechangia kampeni ya Namthamini taulo za kike pakiti 48, ambazo zitakwenda kuwasaidia wanafunzi wa kike wanne kwa mwaka mzima shuleni.

Wawakilishi wa kampuni ya QiPads wakiwa katika ofisi za East Africa TV na East Africa Radio.

Mkurugenzi wa kampuni ya QiPads, Emmanuel Meena anasema wameguswa na kampeni ya Namthamini na waliona ni kitu kizuri kujitolea kwa watoto wa kike ili kuwaweka salama kiafya.

Kampeni ya Namthamini ilizinduliwa mwezi Mei mwaka huu, ikiwa ni msimu wa sita katika kuwasadia wanafunzi wa kike mashuleni tangu mwaka 2017.