Jumatano , 21st Sep , 2022

Kampeni ya Namthamini inayoendeshwa na East Africa TV na East Africa Radio imeanza kugawa taulo za kike kwa wanafunzi, na msimu huu imeanzia katika mkoa wa Mtwara.

Wa pili kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe Dustan Komba akipokea taulo za kike kutoka kwa wafanyakazi wa East Africa TV na East Africa Radio.

Wanafunzi wa shule za sekondari Mikindani na Mitengo zilizopo katika wilaya ya Mtwara, walikabidhiwa taulo za kike pakiti 862.

Pia kampeni hii ikafika katika shule za sekondari Naliendele na Mangamba ambapo wanafunzi wa shule hizo walikabidhiwa taulo za kike jumla ya pakiti 969.

Jumla ya shule nne za sekondari katika wilaya ya Mtwara zilikabidhiwa taulo za kike siku moja ambazo ni Mikindani, Mitengo, Naliendele na Mangamba

Elimu kuhusu hedhi salama ni muhimu katika kuboresha umakini na ufaulu kwa wanafunzi wa kike mashuleni. Kupitia kampeni ya Namthamini licha ya kusaidia wanafunzi taulo za kike, pia hutoa elimu ya hedhi salama kwani itasaidia wanafunzi wa kike namna ya kujitunza na hata wanapokuwa katika siku za hedhi wanakuwa katika mazingira salama na watakuwa wanaendelea na masomo yao bila changamoto yoyote.