Lakini umetafuta namna ya kuepuka na jumbe hizo na umekosa, itakuwaje kama leo nikikupa mbinu na njia rahisi ya kuepukana na kero ya namna hiyo?
Sawa, Kamata simu yako ingia kwenye Application ya WhatsApp baada ya hapo
Gusa vidoti vitatu upande wa kulia, nenda palipo andikwa setting baada ya hapo nenda palipoandikwa Privacy bonyeza alafu shuka chini kabisa mpaka ukutane na chaguo limeandikwa Advanced, alafu chaguo la kwanza ambalo utakutana nalo ambalo limeandikwa Block unknown account message kama iko off iweke on
Baada ya hapo huwezi kuona tena message za usumbufu na hata mtu mwenye namba ngeni akipewa namba yako hawezi kukutumia ujumbe.
Lakini chonde chonde kama wewe ni mfanyabiashara njia hii achana nayo kwani unaweza ukakosa wateja wengi sana ambao watahitaji kuwasiliana na wewe kwa njia ya WhatsApp