Alhamisi , 27th Mei , 2021

Msaikolojia Daniel Marandu amesema ni jukumu la mwanaume kumpa mahitaji muhimu mwanamke wake kama pesa na vitu vidogovidogo kwani ikitokea hapati mahitaji hayo unakuwa unamnyanyasa kijinsia, kihisia na kisaikolojia.

Picha ya Msaikolojia Daniel Marandu

Akizungumzia suala hilo kwenye show ya DADAZ ya East Africa TV Daniel Marandu amesema mwanaume kumpa pesa mwanamke ni sehemu ya upendo pia na suala kutimiza majukumu kwa mwanamke halikwepeki.

"Mwanaume jukumu lake la kwanza kwa mwanamke wake ni kumpa mahitaji yake muhimu, ikitokea hapati atakuwa anamnyanyasa kijinsia, kihisia na kisaikolojia"

"Pesa ni sehemu ya upendo na vitu vidogo vidogo, kwa mwanaume hilo ni jukumu lako kumuhudumia mpenzi wako hilo halikwepeki labda awe hana" ameeleza Daniel Marandu 

Aidha ametaja vigezo vya kumpata mtu sahihi kwenye mahusiano ni kuzingatia imani, pili uaminifu, umpende au akupende na uvumilie madhaifu yake ila vitu kama elimu, muonekano, na kazi vinakuja baadae.