
Gari la Polisi nchini Kenya
Taarifa zinadai kuwa Mwanamke huyo alimshambulia Polisi baada ya kuulizwa kwanini amekaa nje baada ya saa mbili usiku ndipo wakaanza kurushiana maneno kisha akamrukia Polisi na kumshika kichwa chake kwa nguvu na kumng'ata sikio hadi kuling'oa.
Ripoti ya Polisi inaeleza kuwa "Baada ya kugundua amemjeruhi afisa huyo, alikimbilia katika mto unaopakana na Lang’ata na Kibera, Sajini huyo aliokota sikio lake ambalo lilikuwa limeanguka na kuelekea hadi Hospitali ya Nairobi West”.
Aidha ripoti hiyo imeendelea kwa kusema uchunguzi kuhusiana na kisa hicho unaendelea huku Afisa huyo wa Polisi akisubiri kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza sikio lake.
Chanzo : Citizen Tv