Mume achoma godoro la Mama mkwe baada ya kuachwa 

Jumamosi , 29th Mei , 2021

Mwanaume mmoja nchini Kenya anayejulikana kwa jina la Amos Wanjala, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kuchoma godoro na baadhi ya nguo za Mama mkwe wake baada ya mwanaume huyo kuachwa na mke wake.

Godoro

Tukio hilo limetokea usiku wa Mei 28, 2021, baada ya kuvamia nyumba ya Mama huyo anayeitwa Mercyline Wanyama, ambapo alimuamsha na ndipo alipopata upenyo wa kuingia ndani na kuchoma vitu hivyo ambavyo gharama yake ni zaidi ya shilingi elfu 6000 za Kenya.

Imeelezwa kuwa kwa mujibu wa mila na koo ya Wabukusu, Wanjala atapigwa faini kwa kukiuka mila za ukoo huo kwani itabidi mbuzi achinjwe ili afanyiwe utakaso kwa kuwa ni kinyume kwa mtu yeyote kuwashambulia wakwe zake ama kuharibu mali zao.

Chanzo: Tuko Swahili