Wengi sana wanaamini suti ni vazi ambalo haliwezi kutoweka kamwe kama ambavyo mavazi mengine yamekuwa yakipitwa na wakati, hata likivaliwa vipi halipotezi hadhi yake na linaendelea kuwa vazi la kipekee.
Hizi hapa ni faida kadhaa za kuvaa suti;
Kujiamini na kujisikia vizuri; suti ni vazi ambalo ukivaa na kupendeza vizuri unakuwa na uwezo wa kujiamini, kuwa popote au kukutana na yeyote yule kwasababu hakuna unachokihofia katika mavazi, ukijiamini basi unakuwa “comfortable” vilevile.
Inakupa heshima; katika vazi ambalo ukivaa mtu mwingine anakuheshimu bila kujali umri au rika lako basi ni suti, ni kwasababu ni vazi la kipekee linalohitaji unadhifu wa hali ya juu. Kumbuka suti anaweza kuva mtoto mwenye miaka 12 au Mzee mwenye miaka 70 na wote wakapendeza na kuheshimika.
Ni rahisi kupata network kwa watu mashuhuri au taasisi; ni kweli vazi la suti linafanya utazamike kwa jicho la kipekee katika jamii, hivyo una nafasi ya kusikilizwa ama kupokelewa kirahisi sehemu yoyote kutokana muonekano wako. Unaweza kupata connection na watu wakubwa kwenye taasisi au ofisi yoyote n.k.
Inakupa hadhi ya juu katika jamii; kuna msemo wa Kiswahili unasema “mavazi huficha umskini” hivyo unaweza kuwa huna pesa lakini ukivaa suti ukapendeza unaaminika na kuonekana huna shida hizo ndogo ndogo. Unaweza kukopesheka pia.
NB: Asili ya suti ilitokana na Mfalme wa Kiingereza Charles II mnamo mwaka 1666, aliyeiga mfano wa mwenyeji wake wa wakati huo katika mahakama ya Mfalme Louis XIV huko Versailles Ufaransa, ambaye aliamuru kwamba katika Mahakama ya Kiingereza wanaume watavaa koti ndefu, koti ya kiuno (suti) ma kuanzia pale suti likawa vazi la mitindo mbalimbali hadi leo .