Jumatatu , 20th Nov , 2023

Aliyewahi kuwa mkurugenzi mtendaji wa Open A.I amepata kazi ikiwa ni siku chache baada ya kuondolewa kwenye nafasi yake.

 

Mapema ijumaa ya wiki iliyopita taarifa zilisambaa sana mtandaoni kuhusu Sam Altman, kuondolewa kwenye nafasi yake kama mkurugenzi mkuu wa OpenAI

Na muda huo huo aliyekuwa msaidizi wake Ms Murati alichaguliwa na kampuni hiyo kuwa mkurugenzi wa muda.

Leo asubuhi uvumi ukawa mwingi kuhusiana na yeye kurudishwa kwenye nafasi yake, lakini sivyo ilivyo kwa sasa,

Huwenda ukawa unajiuliza nini kilicho pelekea kuondolewa kwenye nafasi hiyo na ikiwa kama mmoja wa waanzilishi wa OPEN.AI inakuwaje anaondolewa?

Kuhusu kuondolewa kwa Sam, kwenye nafasi yake sababu ni nyingi zipo zile za udaku na zipo za ndani.

Moja za ndani ndani, kwenye moja ya chanzo inataja kuwa kutoelewana na bodi ya wakurugenzi juu ya uendeshaji wa kampuni hiyo  kuhusu misingi na maadili ya akili mnemba

Zile za udaku zinaeleza kuwa ile fununu ya kuwa na mahusiano na ndugu yake ndiyo huwenda ikawa sababu. (Hii tuachane nayo kwa sasa)

Sasa inakuwaje mwanzilishi anaondolewa, maamuzi ya nani awepo kwenye maswala ya uendeshaji wa kampuni kwa wenzetu yamekuwa kwenye kiwango cha juu sana,

kwa maana ya unaweza kuwa mmiliki lakini bodi ya wakurugenzi ambao kwa sehemu huwa ni wanahisa wanaweza kukuondoa ikiwa hubebi maono waliyo nayo. 

Unaweza kuhisi Sam, ndiye mkurugenzi wa kwanza kuondolewa kwenye nafasi ikiwa kama yeye pia ndiye muanzilishi, hawa ni baadhi ya waanzilishi waliowahi kuondolewa kwenye nafasi zao.

Steve Jobs kutoka kwenye kampuni ya  Apple Inc,  Jack Dorsey kwenye kampuni ambayo zamani ilikuwa ikifahamika kama Twitter ila X kwa sasa, David Neeleman kutoka JetBlue kampuni ya ndege nchini Marekani,

kwa hapo unaweza kuwa umepata kitu kwa uchache, hiyo yote ilikuwa 9, kumi ambayo ndiyo kubwa zaidi ni kuhusu Sam Altman kuchukuliwa na kampuni ya Microsoft.

Kupitia mtandao wa X mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Microsoft Satya Nadella aliandika kuhusu furaha yao kuwapokea wafanyakazi wapya ambao ni Sam Altman na Greg Brockman, ambao hawa wote wametoka kwenye kampuni ya OPEN A.I (kwa wakati mmoja)

Huyu Greg Brockman, ndiye yule muanzilishi mwenza wa Open A.I lakini aliamua kujiuzulu baada ya kutopendezwa kwa kile alichofanyiwa Sam (kuachishwa kazi ghafla). 

Na hii ndiyo maana ya kusema Sam, hafahamu kuhusu msoto wa kupata kazi. na kwa kukumbusha tu Microsoft waliwekeza kwenye kampuni ya Open A.I hivyo ni wanahisa ambao wanashikilia asilimia 49 kwenye kampuni hiyo.

Na hii ndiyo sababu ya Bing ambayo tulikwisha itolea ufafanuzi ndani ya SUPATECH kuwezeshwa akili mnemba ya ChatGPT 4 tena bure kabisa kwa watumiaji wake wakati kwa mtumiaji wa kawaidi ilihitajika ulipe kiasi kisichopungua elfu 50 kwa mwezi kuipata.

Picha: r.zjlei.com