Jumanne , 7th Dec , 2021

Mwanasayansi wa Nyuki na mazao yake Ismail Selemani, amesema kwamba katika zoezi la kumpanda Malkia, jumla ya madume wapatao 19 huwania kumpanda na wote hupoteza uhai katika zoezi hilo.

Nyuki

Kauli hiyo ameitoa hivi karibuni wakati akizungumza kwenye kipindi cha Mjadala cha East Africa Television, ambapo amesema kwamba Nyuki naye anazo tabia kama za binadamu, kama vile kufikiria, kulisha watoto na wakati mwingine kupanga majukumu.

"Nyuki dume wapatao 19 huwania kumpanda Malkia na wote wanapigana ili kumpanda lakini ni nyuki mmoja tu ndio anayefanikiwa kumpanda Malkia na wote 19 wanakufa, 18 wanakufa katika mapigano ya kumpanda Malkia na mmoja hupata kiharusi na kufa kwasababu anatumia presha kubwa kutoa manii yake,” amesema Selemani.