
Musk ameamua kuchukua msimamo mkali dhidi ya jukwaa kubwa la filamu na vipindi Netflix, ambalo limejizolea umaarufu mkubwa duniani kwa kutoa maelfu ya filamu, tamthilia, vipindi vya watoto na makala mbalimbali.
Nini kimebadilika kwenye Netflix?
Elon Musk anadai kuwa maudhui mengi ya katuni na vipindi vya watoto kwenye Netflix yamejaa ujumbe usiofaa kwa maendeleo ya mtoto wa kawaida. Akitaja moja ya sababu kubwa ni kuingizwa kwa masuala ya mapenzi ya jinsia moja kwenye katuni, jambo ambalo ni kinyume na maadil.
Kwa mujibu wa Musk, wazazi wengi hawajui kile watoto wao wanakiona, na Netflix ambayo wengi huiona kama salama sasa si salama tena.