
Dereva taxi Daniel Kiptanui
Licha ya kutokuwa na taaluma ya Udaktari lakini dereva huyo amepewa sifa baada ya kufaulu kufanya kazi hiyo ya kumsaidia mama huyo kujifungua mtoto wa kiume ndani ya gari lake walipokuwa barabarani.
"Tulimchukua mama pamoja na jirani kukimbia kuelekea Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi, nilijaribu kuongeza kasi lakini dada huyo alisisitiza kuwa ni lazima tusimame gari ili aweze kujifungua na nilikubali"
"Mambo yalikwenda vyema na alijifungua mtoto wa kiume, baada ya kujifungua nilimkimbisha mama huyo na mtoto wake katika hospitali iliyokuwa karibu ambapo walipokelewa, baada ya dakika 20 tuliambiwa wote wako sawa" ameongeza Dereva taxi Daniel Kiptanui
Chanzo : Tuko News
Tazama mwanamke aliyezaa na Barakah The Prince akifunguka mazito