Jumatatu , 4th Jul , 2022

Hedhi salama bado changamoto kwa shule za msingi na sekondari nchini, kwa kutambua hilo Dkt Ibrahimu Ibrahimu wa Hospital ya Sekou Toure, Mwanza leo Julai 3 alifika katika ofisi za East Africa TV na East Africa Radio na kutoa mchango wa taulo za kike pakiti 64.

Dkt Ibrahimu akikabidhi taulo za kike kwa mtangazaji wa East Africa TV, Najma Paul.

Hii ni mara ya pili kwa Dkt Ibrahimu kuchangia kampeni ya Namthamini kwa mwaka huu, Juni 27 Dkt Ibrahimu alifika katika ofisi zetu na kutoa mchango wa taulo za kike pakiti 16.

 

Pia siku ya leo tulipokea mchango taulo za kike pakiti 12 kutoka kwa Abdallah Ngoma ambaye ni msikilizaji mkubwa wa vipindi vya East Africa Radio.

Fahamu kwamba mchango wa Tsh 5,000 utamsaidia mtoto wa kike kupata taulo za kike akiwa shuleni kwa mwezi mzima. Unaweza kuleta mchango wako katika ofisi zetu zilizopo Mikocheni Viwandani. Pia unaweza kutuma mchango kwenye namba yetu ya ofisi 0787633313 yenye jina la East Africa Television.